Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yawinda saini ya Messi

DAvila Messi Kessie Cz Simba yawinda saini ya Messi

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati viongozi wa Simba wakihaha kukisuka upya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao, tayari wameanza kumpigia hesabu winga raia wa Ivory Coast, D’Avila Messi Kessie ambaye inaelezwa huenda mambo yakienda sawa atajiunga na miamba hiyo.

Kamati ya Usajili ya Simba SC chini ya Mtaalam wa hizi kazi za Usajili Crescentius Magori tayari wameanza kufanya sajili za wachezaji wengi, maeneo tofauti ya Afrika.

Simba inahangaika sana kuimalisha eneo lao la kiungo na Ushambuliaji, ambapo kwa kipindi kirefu limekuwa linakosa watu wa maana ambao wanatoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo.

Ukijaribu kuangalia kwa misimu mitatu nyuma, Simba imesajili wachezaji wengi sana eneo la kiungo lakini wote wameshinwa kuonesha makali, Walikuja kina Duncan Nyoni, Pape Sakho, Luis Miquissone, Saido Ntibazonkiza, Sawadogo, Kanoute, Fabrice Ngoma, Babacar Sarr, Hamis Abdallah, Nassoro Kapama na wengine wengi.

D’Avila kwa sasa anakipiga Inova Sporting Club Association ya Ivory Coast, huku nyota huyo akisifika kwa uwezo wa kucheza winga zote yaani kulia na kushoto ambapo msimu uliopita alifunga mabao 11 na kuasisti sita.

Endapo kama akitua ataungana na Kramo Aubin aliyesajiliwa msimu uliopita, lakini hakutumika kwa sababu ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu, japo kwa sasa amepona kabisa.

Tayari Simba imekamilisha usajili wa Winga wa Kimataifa wa Power Dyanamos Joshua Mutale na mchezaji wa DR Congo Elie Mpanzu ambao wote watatambulishwa muda wowote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: