Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yanasa saini ya jembe la ASEC

IMG 4553.jpeg Simba yanasa saini ya jembe la ASEC

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba juzi ilianza kutangaza rasmi mastaa wapya watakoitumikia timu hiyo msimu ujao, ila habari njema zaidi kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo ni kunaswa kwa saini ya winga wa maana anayejua kazi ya kukimbia mithili ya kiberenge kutoka klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Mabosi wa klabu hiyo juzi saa 7 mchana ilimtangaza kiungo mshambuliaji Leandre Willy Onana akiwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa kwa ajili ya msimu ujao, lakini ikiwa tayari imeshamnasa winga Kramo Aubin kutoka ASEC aliyepewa mkataba wa miaka miwili kumtumikia Mnyama.

Onana alikuwa akiichezea Rayon Sports ya Rwanda na msimu uliopita alikuwa Mfungaji na Mchezaji Bora akiifungia timu hiyo mabao 17 amepewa mkataba wa miaka miwili kama Mwanaspoti lilivyowaripotia mapema kabla ya utmbulisho huo wa jana mchana.

Kwa ishu ya Aubin, ni kwamba Simba ilimsafirisha mtu kimyakimya kumfuata Kramo nchini kwao kisha kumsainisha mkataba huo hukohuko Ivory Coast ili kujihakikishia huduma za winga huyo baada ya kusikia ana ofa nyingi mezani zikiwemo kwenda Afrika Kaskazini.

Winga huyo anayemudu kutumia miguu yote kwa ufasaha kama humjui ni kwamba aliwahi kuwadhuru Simba mara mbili ambapo msimu wa juzi wekundu hao walipokutana na Asec alihusika kwenye mabao mawili ya kwanza ya timu yake katika mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Hapa nyumbani katika mchezo wa kwanza, Simba ikicheza dhidi ya Asec ikiwa ni mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na Kramo ndiye aliyemsababishia balaa beki Joash Onyango akizuia pasi ya Mkenya huyo kisha mpira kuunasa Stephanie Aziz KI aliyewapunguza mabeki wa wekundu hao kisha kwenda kumfunga kipa Aishi Manula wakisawazisha bao.

Kama haitoshi kule ugenini akaifunga bao la kikatili Simba bao la kwanza dakika ya 53 akiwazidi akili mabeki wa wekundu hao ambapo maumivu hayo yakawalazimisha mabosi wa Simba kumpandia ndege, ili kumalizana naye aje kuvaa uzi wa rangi nyekundu na nyeupe.

Msimu uliopita kwenye mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho, Kramo aliupiga mwingi na kufunga mabao manne katika mechi tatu kati ya sita za hatua hiyo na imu hiyo kutolewa nusu fainali na USM Alger ya Algeria iliyobeba ndoo kwa faida ya bao la ugenini mbele ya Yanga.

Usajili wa winga huyo unamaanisha kwamba sasa Simba imepata mtu muafaka katika kushambulia kutoka pembeni wakiwa wamefanyia kazi mapendekezo ya kocha wao Robert Oliveira 'Robertinho' ambaye alitaka kuletewa winga anayejua kazi yake.

Simba pia itakuwa imetuliza nafsi baada ya kumkosa winga Mkongomani, Maxi Nzengeli waliyemvamia ghafla wakitaka kupindua meza mbele ya watani wao wa Yanga, ambayo ilifanikiwa kunasa saini yake kwa baada ya kupambana kwelikweli.

Aubin mwenye miaka 27 alijiunga na Asec mwaka juzi akitokea FC San Pedro pia aliwahi kukipiga Africa Sports iliyomsajili akitokea Asec aliyoichezea hapo mwaka 2015.

Mbali na Aubin, Simbna pia inahusishwa kumsainisha beki wa kati kutoka Cameroon, Che Fondoh Malone JR wa CotronSport ambaye anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Joash Onyango aliyekomaa kutaka kuondoka Msimbazi ili aungae na Kennedy Juma na Henock Inonga waliopo muda mrefu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: