Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaleta kipa la Ulaya na Mzawa

Hussein Mzawa Simba yaleta kipa la Ulaya na Mzawa

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mabosi wa Simba wajanja sana, wakati leo ni Simba Day, wenyewe wamepanga kuwafanya sapraizi mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwatambulisha makipa wawili wapya akiwamo aliyecheza soka lake lote Ulaya, licha ya kuwa na uraia wa DR Congo, anayechukua nafasi ya Mbrazili Jefferson Luis.

Jefferson aliyesajiliwa kutoka klabu ya Resende ya Brazili alitemwa siku chache kutokana kilichoelezwa ana majeraha yatakayomweka nje na kufanya mabosi wa klabu hiyo kuingia sokoni kusaka kipa mpya na atimaye turufu imemwangua Lionel Mpasi-Nzau.

Kipa huyo mwenye urefu wa futi sita na mzaliwa wa mji wa Meaux, Ufaransa amesajiliwa kutoka klabu ya Daraja la Pili ya Ufaransa iitwayo Rodez AF, huku pia akiidakia timu ya taifa ya DR Congo.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba zinasema kipa huyo aliyewahi kucheza timu ya vijana za PSG U-19, Toulouse pamoja na timu za taifa za vijana za Ufaransa U16, U17 na U18 amepewa miaka miwili na leo atatambulishwa rasmi sambamba na kipa mzawa Hussein Abel aliyewahi kuichezea KMKM, tanzania Prisons na KMC. Nzau anakuwa mchezaji wa nne kutoka DR Congo katika kikosi kipya cha Simba, akiwamo Henock Inonga, Jean Baleke na Fabrice Ngoma.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: