Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yakubali mziki wa Yanga yawaachia Aziz Ki

STEPHANE AZIZ KI Yanga Aziz Ki

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: Global Publishers

Mabosi wa Simba wamejitoa kwenye vita ya kuwania saini ya mshambuiliaji wa Asec Mimosas ya Ivory Coast, Mbukinabe, Aziz Ki anayewindwa na Yanga katika usajili wa msimu ujao.

Awali, Simba ndio ilikuwa ya kwanza kumfuata Ki kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya awali baada ya kumuona katika Kombe la Shirikisho Afrika walipokutana kundi moja.

Yanga wakatokea kwa mbele na kumfuata mshambuliaji huyo kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo ambayo yamemshawishi kuwa tayari kusaini Jangwani.

Mmoja wa mabosi wakubwa wenye ushawishi wa usajili Simba, ameliambia Championi Ijumaa kuwa wamefikia hatua ya kuachana na mshambuliaji huyo baada ya kupata taarifa za Yanga kumfuata.

Bosi huyo alisema kuwa kwa levo ambayo wamefikia Simba hivi sasa siyo ya kugombania mchezaji, kwani wao wenyewe ndio wanataka kusajiliwa na timu hiyo kutokana na mafanikio waliyoyapata ndani ya misimu miwili kimataifa.

Aliongeza kuwa hawataki kushindana kuwania usajili wa wachezaji na timu yoyote ndani ya nchi, hivyo basi watarudi kufanya mazungumzo na mshambuliaji kama wakishindwana naye.

“Tumewaachia Yanga waendelee kufanya mazungumzo na Ki, ni baada ya kusikia wamemfuata na wao kwa ajili ya kuzungumza naye.

“Yanga wamekuwa na tabia ya kumfuata kila mchezaji ambaye sisi tunamhitaji, hivi sasa wamerudi tena kwa Ki baada ya kusikia tumeanza mazungumzo.

“Tutarejea kufanya naye mazungumzo Ki kama wakishindwana na Yanga, lakini kwa sasa tumewaachia wao kwanza,” alisema bosi huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alipotafutwa alisema: “Simba huwa hatufanyi mambo kwa kubahatisha na kupiga kelele kama hao wengine, sisi tutasajili wachezaji wa daraja la juu kabisa, watakaoifanya timu kuwa imara na kuhusu Ki huu sio muda wake.”

Chanzo: Global Publishers
Related Articles: