Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunguka Manula, Tshabalala, Baleke kuondoka

Jean Baleke Tatu Simba yafunguka Manula, Tshabalala, Baleke kuondoka

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari wa Simba SC amefunguka kuwatoa hofu wadau na mashabiki wa klabu hio kuhusu kuondoka kwa wachezaji nyota ambao wamekuwa wakitajwa kuhusishwa zaidi na usajili katika vilabu vingine.

Ameeleza kuwa wachezaji wote watakao hitajika na klabu hio watasalia hata kama mikataba yao itakuwa imekamilika taratibu mpya itafuata kuwabakisha.

“Unapokua na wachezaji wenye ubora mkubwa tegemea tetesi nyingi kipindi cha usajili Mohammed Hussein anatakiwa na timu za South Afrika, Manula anukia Azam Fc, Baleke anatakiwa na timu za Ulaya.

“Niwathibitishie Wanasimba hakuna mchezaji ambae yupo kwenye mipango yetu ataondoka, wale waliomaliza mkataba na tunawahitaji watasalia, maboresho tunayoyafanya ni pamoja na kuwabakisha wale tunaowahitaji.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: