Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yachomoa viungo wawili Yanga

Mukoko Yacouba Simba yachomoa viungo wawili Yanga

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imeanza mazungumzo na viungo wa zamani wa Yanga, Mkongomani, Mukoko Tonombe anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo na Mburkinabe Yacouba Songne ambaye yupo Ihefu kwa sasa.

Songne aliachwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili msimu huu, akatua Ihefu akiwa mchezaji huru akisaini mkataba wa miezi sita unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Simba ipo katika mikakati ya kukisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, na tayari wapo baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na timu hiyo akiwemo kiungo wa Rivers United ya Nigeria, Joseph Onoja.

Taarifa ambazo tumezipata, kutoka ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kama mazungumzo hayo yakienda vizuri, basi viungo hao msimu ujao wataonekana wakivalia jezi zenye rangi nyekundu na nyeupe.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, wachezaji wenyewe wameonesha nia kubwa ya kujiunga na Simba, kama wakihakikishiwa dau na mshahara mzuri kutoka kwa uongozi wa timu hiyo.

Aliongeza kuwa, Simba wamepanga kukiboresha kikosi chao katika baadhi ya maeneo, kati ya hayo ni kiungo mkabaji baada ya Ismail Sawadogo kushindwa kuonesha ubora wake na kiungo mshambuliaji atakayetokea pembeni.

“Tumepanga kukifanyia maboresho makubwa kikosi chetu baadhi ya sehemu ambazo ni kiungo mkabaji na ushambuliaji.

“Wapo baadhi ya wachezaji tuliokuwa nao katika mazungumzo ambayo kama yakienda vizuri, basi tutawasajili, kati ya hao ni Yacouba Songne na Mukoko Tonombe waliowahi kuichezea Yanga.

“Kwa sasa tupo katika mazungumzo nao, kama yakienda vizuri basi tutawasajili, kwani tunawaona ni wachezaji wenye uzoefu wa kucheza Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa,” alisema mtoa taarifa huyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia hilo na kusema kuwa: “Uongozi upo makini ukifuatilia mashindano ya kimataifa yanayoendelea kwa ajili ya kuangalia wachezaji.

“Tayari wapo baadhi ya wachezaji ambao uongozi unawafuatilia kwa ukaribu kujua ukomo wa mikataba yao, kama mazungumzo yakienda vizuri, basi tutawasajili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: