Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walivyotaka kupora beki Yanga

Boka Simba walivyotaka kupora beki Yanga

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imebainika kuwa taarifa nyeti kutoka katika klabu ya Simba SC kuwa ilitaka kumchukua Mchezaji FC Lupopo, Chadrack Boka ambaye inaripotiwa kuwa ameshamalizana na klabu ya Yanga SC.

"Sikuwahi kufanya mazungumzo nao (Simba) kabla, lakini kocha wangu mmoja alinitafuta na kuniambia watu wa Simba wanakutafuta. Akawapa namba zangu wakanipigia lakini sikuwa na maongezi nao marefu.

"Niliwaambia kwamba tayari nilishasaini mkataba wa awali na Yanga SC, wakaniambia nisiende huko watajua namna ya kumaliza hilo. Nikawaambia wawatafute wenyewe Yanga au wamtafute Rais wa Yanga yeye ndiye aliyekuja huku kuongea na mimi," amesema Chadrack Boka, Mchezaji wa FC Lupopo.

"Kweli tulipokea simu za watu wa Simba SC wanasema wanajua kwamba Boka bado ni mchezaji wa FC Lupopo na wanataka kutupa pesa mara mbili ya ile Yanga wanataka kutoa kama tukikubali kufanya biashara"

"Tumewaambia hakuna namna mambo yanaweza kubadilika kwa kuwa kila kitu kimemalizika muda mrefu, kama wao bado wanamtaka mchezaji wasubiri afike Tanzania wataongea na watu wa Yanga.

"Lupopo hatuzuii kufanya biashara, zipo timu ambazo hatuwezi kufanya nazo biashara hata za mchezaji mmoja na hizo timu zipo hapa Congo, lakini nje ya hapa tunaweza kufanya biashara na timu yoyote.

"Kwa hili la Boka hakuna njia tunaweza kupindua mambo kwa kuwa kila kitu kimemalizika vizuri. Yanga walikuja hapa tukaongea na Rais wao na baadae Rais wetu Bwana Kyabula Jacques amekuja Tanzania, wakatuma tena mtu hapa tukamaliza hiyo biashara. Kitu kilichobakia ni Yanga kumlketa mchezaji huko Tanzania kwa muda watakaoona unafaa," amesema Donat Mulongoy, Karibu Mkuu wa klabu ya FC Lupopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: