Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba walifika fainali ya CAF Cup, CAFCC ni kubwa - Hersi

Yanga Msad.jpeg Eng. Hersi akisalimiana na Waziri wa Michezo, Pindi Chana

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amesema kuwa watani zao wa jadi, Simba hawajawahi kuingia nusu fainali ya mashindano makubwa Afrika kama CAFCC, badala yake waliingia fainali ya michuano ya CAF Cup ambayo ni madogo kwa hadhi.

Kauli hiyo ye Hersi imekuja mara baada ya kutinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika wakati huo Simba wakidai walishawahi kufanya hivyo miaka ya nyuma.

"Niweke sawa kulikuwa na kombe linaitwa CAF Cup kombe hilo ndio wenzetu walifika Fainali, kulikuwa na shindano lingine linaitwa CAF Winners Cup (Kombe la Washindi).

"Mashindano haya yaliunganishwa mwaka 2004 yakatengeneza CAF Confederation Cup hili ni kombe kubwa liliounganisha mashindano mawili (CAF Cup & CAF Winners Cup).

"Yanga ndio Klabu ya kwanza kutoka Tanzania kushiriki mashindano haya kwenye ngazi ya Nusu Fainali, lakini Yanga iko mguu mmoja kuelekea Fainali, hajawahi kushiriki yoyote kutoka Tanzania kombe hili hatua ya Nusu fainali," amesema Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: