Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba vs Fountain Gate bado hatihati kuchezwa

Simba Vs Fountain Gateeeeeeeeee Simba vs Fountain Gate bado hatihati kuchezwa

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha Fountain Gate kimeanza safari ya kutoka Lindi kuja jijini Dar es Salaam kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili, huku ikiwa bado haijajua hatma kama mechi hiyo itachezwa au la.

Timu hiyo ilishindwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Namungo, Agosti 17 kwenye Uwanja wa Majaliwa Ruangwa, Lindi kwa sababu ya kutokamilisha taratibu za uhamisho wa wachezaji kutokana na kikosi hicho kufungiwa kutosajili.

Fountain ilifungiwa kusajili na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) wakati huo ikiitwa Singida FG kutokana na baadhi ya wachezaji kuidai akiwemo aliyekuwa nyota kutoka Mbrazili, Rodrigo Figueiredo Calvalho.

Hata hivyo, uongozi wa Fountain chini ya ofisa mtendaji mkuu (CEO), Kidawawa Tabitha amesema, kila kitu wameshakamilisha kwa ajili ya kumlipa mchezaji huyo na kilichobaki ni Mbrazili huyo kuthibitisha kupokea fedha hizo ili waruhusiwe rasmi.

"Ni kweli tumeshalipa kila kitu na sasa tunachosubiria ni mchezaji au wakala wake kuthibitisha pesa tuliyomtumia ili FIFA watufungulie, tunashukuru mamlaka ya soka hapa nchini wanalitambua hili na wako bega kwa bega na sisi," amesema.

Kidawawa ameongeza, uhamisho wa wachezaji wote walikamilisha kwa wakati na kuingiza katika mfumo hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linatambua hilo, na ndio maana wamekuwa karibu nao ili kumaliza changamoto hiyo inayoendelea kwao.

Akizungumzia suala hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo amesema, hakuna taarifa mpya ila wao kwa kushirikiana na TFF watavuta subra ili jambo hili limalizike kwa wakati kwa sababu hawataki kuvuruga ratiba ya Ligi.

"Lengo letu ni kuhakikisha ratiba tuliyoitoa inaisha kwa wakati japo tunatambua tumeanza na changamoto hii ila ni imani yetu kila kitu kitaenda kama tulivyokipanga, kwa sasa tunaendelea kuvuta subra ili tuone kile kitakachojitokeza mbele."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: