Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba na Warundi ni 'pete na kidole'

Saido 1 Goal Saido Ntibanzokiza

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni ukweli usiopingika, soka la Tanzania limekuwa kivutio kwa nyota wa kigeni tangu miaka ya 1970 hadi leo, ikishuhudiwa mastaa mbalimbali kutoka mataifa tofauti wakimiminika kuja kucheza nchini.

Utabisha nini, wakati Fredy Mayaula Mayoni kutoka Zaire (DR Congo ya sasa) alikipiga Yanga 1970 na kubahatika kufunga mara mbili kwenye pambano la Kariakoo Derby alipoizamisha Simba kwa 2-1.

Huyu ndiye mchezaji wa kwanza wa kigeni kucheza soka la kulipwa nchini, kabla ya kugeukia muziki na kupata umaarufu mkubwa duniani. Kwa sasa ni marehemu.

Makocha wakubwa wa kigeni kutoka barani Ulaya, Latin America sambamba na wa nchi za Kiafrika wamekuwa wakiingia na kutoka nchini tangu miaka hiyo hadi leo kwa ajili ya kufundisha klabu mbalimbali na timu za taifa, kuthibitisha soka la Tanzania linaeleweka nje ya mipaka.

Profesa Victor Stansleascu kutoka Romania, Tambwe Leya kutoka Zaire (sasa DR Congo) na Nabi Kamala (Guinea) walikuja kufundisha Simba na Yanga miaka ya 1970 kisha kutuatiwa na wengine, huku pia ikishuhudiwa wachezaji mahiri kutoka nje wakimimbika zaidi miaka ya 1990.

Utasema nini, wakati kuna majina makubwa yalipita nchini kama kina Nonda Shaaban 'Papii', Ngandou Ramadhani, Constantine Kimanda, William Fahnbulleh, Kipre Tchetche na wakali wengine walipita kabla ya sasa Fiston Mayele, Prince Dube, Saido Ntibazonkiza, Jean Baleke, Idris Mbombo, Bruno Gomes na Djigui Diarra kukimbiza katika Ligi Kuu Bara.

Rekodi zinaonyesha, Yanga imekuwa na zali na nyota wa kigeni na hata makocha kutoka DR Congo, ilihali kwa upande wa Simba imekuwa na kismati na wachezaji kutoka Burundi.

Simba ni moja ya klabu iliyowahi kukimbiliwa na wachezaji Warundi, licha ya kwamba kwa miaka ya karibuni imekuwa ikibadilisha kwa kusajili nyota kutoka mataifa mengine yakiwamo ya Zimbabwe, Ghana, Zambia, Kenya, Uganda na hata DR Congo.

Hapa chini ni orodha ya kikosi na makocha waliowahi kutua au waliopo Msimbazi kutoka Burundi, hata kama baadhi yao hawakupata mafanikio makubwa kulinganisha na nyota wenzao wa Kikongo waliopita au waliopo Jangwani. Ieleweke hata Yanga imekuwa ikikimbiliwa na wachezaji wa kutoka taifa hilo la Burundi, lakini kimafanikio halingani na ile ya watani wao.

Mmoja ya nyota wa mwanzo kabisa kusajiliwa na Simba kutoka Burundi alikuwa ni, Damian Morisho Kimti aliyetua miaka ya 1990 na kuwa sehemu ya mastaa walioisaidia timu hiyo kucheza fainali ya michuano ya Kombe la CAF 1993, japo baadaye ilikuja kuelezwa alikuwa ni mzawa na kuzima zile kelele mshambuliaji huyo mfupi aliyefariki dunia Machi, 2020 alikuwa ni Mrundi. Endelea nayo....!

MACKENZIE RAMADHANI Huyu ni mmoja wa makipa tegemeo waliowahi kukipiga Msimbazi kwa mafanikio makubwa. Kipa huyu aliyekuwa mashoto, alisajiliwa na Simba miaka ya 1990 na kuungana na makipa wengine hodari wa Kitanzania akiwamo Idd Pazi 'Father' na kuifanya timu hiyo iwe na machaguo mengi kwenye nafasi ya kulinda milingoti mitatu.

Hadi anaondoka Simba, Mackenzie alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichobeba mataji kadhaa yakiwamo ya Ligi Kuu Bara 1990, Ligi ya Muungano na Kombe la Kagame, japo alipoteza umaarufu baada ya kusajiliwa kwa Mohammed Mwameja kutoka Coastal Union aliyepishana na Pazi aliyeenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na baadaye akatemwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: