Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba kuanza kuwaanika wanaotemwa

SIMBA 388 1140x640.png Simba kuanza kuwaanika wanaotemwa

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuanzia Jumatatu ijayo, Juni 19, 2023 itaanza kutangaza majina ya wachezaji wake ambao wataachana nao msimu ujao kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi la timu hiyo.

Hayo yameelezwa leo na Msemaji wa Simba, Ahmed Ally wakati akizungumzia mpango mkakati wa klabu hiyo kuboresha benchi lake la ufundi pamoja na kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa soka.

“Jana tumeachana viongozi waliokuwa kwenye benchi letu la ufundi ambao tumeachana nao, wamefanya kazi nzuri kwenye klabu yetu na tunawashukuru, ni wakati wa kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi chetu kwa sababu msimu ujao tunataka kufanya mambo makubwa zaidi.

“Ni misimu miwili hatujapata taji lolote kwa hiyo ni wakati wetu sasa kujipanga na kuirejesha Simba tishio kwenye ramani yake.

“Bodi ya Klabu ilikuwa ikipitia ripoti ya mwalimu na mapendekezo yake, na kuanza kujadiliana na wachezaji ambao mwalimu amependekeza waondoke klabuni, tayari tumeshaanza nao mazungumzo ili tuachane kwa amani na sio kwa ugomvi.

“Mambo haya yanakwenda vizuri, tunaamini kuanzia Jumatatu tutaanza kuachia majina ya wachezaji ambao tunaachana nao ili sasa tuanze kusajili na kuboresha kikosi chetu kiwe imara zaidi tayari kwa mapambano ya msimu ujao," amesema Ahmed.

Mpaka sasa Simba aimeshawapa mkono wa kwa heri watu wanne kutoka kwenye benchi lao ufundi wakiwemo Kocha wa makipa Zakharia Chlouha, kocha wa viungo Kelvin Mandla na mtaalamu wa viungo Fareed Cassiem na kocha wa timu ya wanawake Charles Lukula sambamba na mchezaji wao, Augustine Okrah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: