Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba inasubiri Yanga wajichanganye tu!

Simba SC Uganda 1 1140x640 Simba inasubiri Yanga wajichanganye tu

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imeshinda mchezo wake wa 17 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 3-0 katika mchezo ambao ulionekana wa upande mmoja.

Simba haikuwa na kazi ngumu mbele ya Mtibwa iliyoonyesha kuwa dhaifu na kushindwa kubisha lolote mbele ya Wekundu wa Msimbazi, ambao ushindi huo unaifanya kusubiri makosa ya Yanga inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi nane, ambayo nayo jana imeibuka na ushindi dhidi ya Geita Gold.

Dakika 45 za Baleke

Mchezo huo ni kama Simba ilikuwa ‘inakula pweza gizani’, kwani hakuna mashaka kwamba utakutana na mfupa, dakika 45 za kwanza tu zilitosha kuihakikishia ushindi huo kwa mabao yote matatu kupatikana.

Mabao hayo ya Simba yalifungwa na muuaji mmoja, Jean Baleke akifunga la kwanza dakika ya tatu kwa mguu wa kulia, lakini mengine mawili akiyafunga kwa kichwa chake akijihakikishia ‘hat-trick’ yake ya kwanza ndani ya Msimbazi,

Mtibwa wako hoi

Hakuna idara ambayo Mtibwa ilionyesha uhai, timu yao haikuwa na ubora wa kuzuia, ilifanya makosa mengi ambayo yalihitaji makosa ya washambuliaji wa Simba na viungo tu wasifunge zaidi.

Ukiangalia eneo la kiungo nalo hali ilikuwa mbaya, ilitengeneza nafasi kubwa ya wazi kuifanya Simba kutawala eneo hilo ikiwatumia Mzamiru Yassin , Sadio Kanoute kuzima mipango yao, huku juu akiwa Said Ntibazonkiza ‘Saido’ na Clatous Chama kupanga mashambulizi.

Simba ilistahili ushindi mkubwa zaidi

Simba kushinda 3-0 pengine ulikuwa uamuzi wao kama si wachezaji wake kukosa umakini, kwani ilistahili ushindi mkubwa zaidi ikipoteza nafasi nyingi za kufunga, hasa kipindi cha pili.

Mabao matatu ambayo Mtibwa iliyaruhusu juzi yamiweka timu hiyo katika msimamo wa timu iliyoruhusu mabao mengi kuliko hata Polisi Tanzania, ambayo inashika mkia, ikiruhusu mabao 38.

Hii ni idadi kubwa ambayo inawafanya Mtibwa kutambua eneo lao la ulinzi lipo katika hali mbaya zaidi, huku washambuliaji nao wakifunga 26 pekee.

Inawezekana makipa wa Mtibwa wakaonekana kuwa katika kiwango kidogo, lakini ni wakati wa kuangalia pia ubora wa mabeki wao na hata eneo la viungo wakabaji.

Msikie Baleke

Akizungumzia mchezo huo, Baleke alisema kwake ni mafanikio makubwa kufunga hat-trick katika mchezo wa Ligi Kuu na kwa timu yake, kasi ambayo anataka kuendeleanayo kimataifa.

“Nimefurahi kufunga na kuipata ushindi timu yangu, mabao haya yameniongezea morali na ari ya kujiamini zaidi na nataka niendelee kufanya hivi kwenye kila mechi.

“Awali sikuwa na muendelezo mzuri, lakini sababu kubwa ni uzoefu, nimeingia kwenye timu katikati ya msimu, hivyo nilihitaji muda wa kuzoeana na kujua timu inachezaje na sasa angalau tumezoeana na naamini tutafanya makubwa zaidi,” alisema Baleke.

Mchezaji huyo pia amemtaja mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kama mmoja wa nyota wanaoweza kuwa vinara wa mabao msimu huu, huku Baleke akitaka kufikisha japo 10 tu ya ligi.

Baba ubaya huyu hapa

Beki wa kushoto na nahodha wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ alisema kukosa kwao umakini katika dakika 45 za kwanza ndiyo zilizowatengenezea ushindi wapinzani wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: