Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba hii, hakuna kulala!

Simba SC Kwa PD Simba hii, hakuna kulala!

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Simba, Robert Oliveira 'Robertinho' amesema atatumia siku 16 za mapumziko kukiimarisha zaidi kikosi chake na kuongeza makali kwenye idara.

Amesema siku hizo 16 kwake atazitumia kikamilifu kuhakikisha wanarejea uwanjani wakiwa na makali mara mbili zaidi ya sasa.

Robertinho ametoa kauli hiyo huku Simba ikiwa inaongoza ligi kwa kuwa na pointi sita baada ya kucheza michezo miwili ya Ligi Kuu Bara msimu huu huku wakiwa wamefunga jumla ya mabao sita na kuruhusu mabao mawili.

Akizungumza nasi, Robertinho amesema kwa kuwa wanaenda kwenye mapumziko mafupi ya Ligi Kuu kwa ajili ya kupisha michezo ya timu za Taifa, amepanga kuendelea na programu zake za mazoezi.

Amesema anahitaji muda mwingi wa kuendelea kukisuka kikosi cha timu yake hiyo huku kundi la pili ambalo lilichelewa kujiunga kwenye 'Pre Season' wanaenda sawa na kundi la kwanza lililowahi kwenye maandalizi yao Uturuki.

"Nimetoa mapumziko kwa wachezaji ambayo yatachukua siku nne na kurejea kikosini, baada ya hapo tutatumia siku 16 kujiandaa, unajua wakati wa maandalizi yetu Uturuki kuna wachezaji walichelewa kufika sasa tutatumia siku hizi kuweka mambo sawa na kuongeza makali yetu kwenye nafasi zote," amesema Robertinho.

Alisema baada ya siku hizo kikosi chake kitarejea kwenye michezo yake ya ligi kuu kwa kasi na nguvu zaidi.

"Nadhani maboresho ya muda huo yatasaidia kuwa na timu ya ndoto zetu wanasimba, tutarejea na nguvu na ubora zaidi," amesema Robertinho.

Aidha, amesema mara zote amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kuzingatia mazoezi na kuwa na nidhamu nayo ili kuwa imara zaidi na kuwa na timu ya ushindani kwa sababu anahitaji kupata ushindi kila mechi na kucheza mpira mzuri.

Robertinho amesema kipindi hiki ligi ikiwa imesimama atatumia pia kutengeneza muunganiko wa kila nafasi ikiwemo safu ya ulinzi ili kuwa imara na anapokosekana Che Fondoh Malone katika timu hiyo kuwe na mtu anayeweza kuziba nafasi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: