Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba baba wa historia Tanzania

Mashabiki Mkapa Simba.jpeg Simba baba wa historia Tanzania

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Leo ndio leo pale Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Simba Sports Club ‘Wenye Nchi’ watakuwa na jambo lao na Unyama ni mwingi sana.

Unaambiwa Mama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani atakuwa mgeni rasmi. Hii nayo ni histoaria mpya na uwanja uko ‘fulu hausi’.

HISTORIA YA SIMBA

Zamani kulikuwa na timu iliyoitwa Jangwani Boys- jezi zake zilikuwa kama mnyama pundamilia- nyeupe na nyeusi. Baadaye ikabadili jina na kujiita Navigation na kubadili tena na kujiita New Young Boys.

Mwaka 1936 baadhi ya viongozi (sio wachezaji kama inavyopotoshwa) walitoka katika New Young Boys na kwenda kuanzisha timu yao baada ya kushindwa kuelewana.

Waliita timu yao Eagles na baadaye Sunderland. Mwaka 1971 ikaitwa Simba Sport Club

Maskani yake ya kwanza yalikuwa Mtaa wa Congo na Mchikichi Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Mtaa wa Msimbazi, ikiweka historia kibao katika nchi hii kuliko klabu nyingine yoyote.

Achana na uanzilishi wa matamasha ya kutambulisha wachezaji kama Simba Day klabu nyingi zimeiga. Simba pia imeasisi mtindo wa kuwatangaza wachezaji wapya katika mitandano ya kijamii kwa kutaja muda maalumu. Klabu imekuwa na mambo mengi ya kihistoria mengine ni kama yafuatavyo.

SUNDERLAND VS NEW YOUNG BOYS

Mwaka 1938 ndipo upinzani wa jadi ulipozaliwa rasmi, mchezo wa kwanza timu hizo zilipokutana katika kugombea Heavy Cup. Heavy alikuwa mwalimu wa shule ya serikali na watoto wengi wa Sunderland walitoka katika shule hiyo. Katika mchezo huo uliocheza karibu na Hospitali ya Muhimbili, Sunderland ilishinda 3-1 dhidi ya New Young Boys. Tangu hapo utani ukaongezeka na kuwa mkubwa zaidi hadi leo hii.

Mwaka 1935 New Young Boys ilibadili jina na kujiita Young African na kuvaa rasmi jezi za njano.

IMEMNYANYASA SANA MTANI

Hapa nchini Simba ndiyo klabu inayoongoza kumpa mtani wake kichapo cha mabao mengi katika mchezo mmoja.

Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0 ni takribani miaka 46 rekodi hiyo ikiwa haijavunjwa.

Julai 2 1994, Simba iliipa kisago Yanga cha mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa (Uhuru) jijini Dar es Salaam.

Kama haitoshi Mei 6, mwaka 2012 Simba iliinyuka Yanga mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Julai 13, Simba tena iliiadhibu Yanga kwa kuifunga mabao 4-1 kwenye nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).

WA KWANZA KUVAA JEZI, VIATU

Mwaka 1938 ikiitwa Sunderland ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga Bandari ya Dar es Salaam.

Mwaka 1941, Sunderland ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya Jeshi la Maji la mkoloni la Afrika Mashariki.

YA KWANZA KUPANDA NDEGE KUMILIKI BASI

Mwaka 1959, kabla ya Uhuru wa Tanganyika, Sunderland ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege. Ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.

Kama haitoshi mwaka 1965, Sunderland ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.

1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza kumiliki basi lake na mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza nchini kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati.

Pia, mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika).

HISTORIA YA DUNIA

Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani mabao 4-0 na kwenda ugenini kushinda 5-0 dhidi ya Mufulira Wanderers ya Zambia Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Simba ndio mabingwa wa muda wote wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (makombe sita).

Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi. Zamalek ilikuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo

BINGWA WA HAMASA

Simba imefikia robo fainali ya mashindano ya Caf, msimu wa 2018/19 na 2020/21 ilifika ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na msimu wa 2021/22 ikifika hatua hiyo katika Kombe la Shirikisho Afrika. Pia, msimu wa 2022/23 imefika hatua hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika kipindi hiki kila timu alitamani kuwa kama Simba, hamasa ilikuwa kubwa kiasi cha kuanza kuziamsha klabu nyingine kujipanga.

INA MATAJI MENGI

Simba inamiliki makombe mengi ya jumla kuliko klabu nyingine Afrika Mashariki. Simba ina mataji rasmi 58 kwenye makabati yao kama Simba. Ndio klabu iliyoiwakilisha nchi kwa mafanikio zaidi kuliko nyingine yeyote nchini.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: