Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba, Yanga watajwa Bungeni

Simba Yanga Dg Simba, Yanga watajwa Bungeni

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amezipongeza timu za Simba na Yanga za Dar es Salaam kwa kufikia robo fainali ya michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Klabu ya Simba inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Klabu ya Yanga ipo Kombe la Shirikisho.

“Ninavipongeza sana vilabu hivyo kwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

"Ni matumaini yetu sote kuwa vilabu hivyo na vingine vinavyoshiriki mashindano ya kimataifa vitaendelea kujituma na kupambana ili vikombe vya ushindi vije nyumbani," amesema Majaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: