Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Yanga? Lazima waache pointi

Mayele Baleke Dd Mayele vs Baleke

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umesema kuwa kwa sasa hauna hofu na timu yoyote kwani tayari wameshapita katika hatua hiyo ya kuwaogopa wapinzani kutokana na ukubwa walionao kwa sasa huku wakiwataka wapinzani wajiandae.

Simba wanatarajiwa kukutana na Yanga April 16, katika mchezo wa ligi kuu ukiwa mchezo wa mzunguko wa pili huku pia wakiwa na uwezekano mkubwa wa kukutana katika fainali ya kombe la FA kama wote watafuzu katika nusu fainali.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema: “Kwa sasa sisi Simba tumeshavuka katika levo za kuwahofia wapinzani, Simba ya sasa ipo tayari kupambana na mpinzani yeyote ambaye yupo mbele yetu.

“Tunafahamu kuwa tuna ratiba ngumu ya kucheza mechi ya mtani kisha kimataifa dhidi ya Wydad Casablanca, nataka niwaambie kuwa kila mchezo tutacheza kwa malengo ya kupata ushindi na sio jambo lingine.

“Hakuna ambapo tutasema kuwa tunahitaji sare wala kupoteza hakuna kitu kama hicho ambacho sisi tunafikiria ni kupata matokeo katika kila mchezo ambao tutacheza ulio mbele yetu hivyo wapinzani ambao tunacheza nao wajiandae,” alisema kiongozi huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: