Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba SC kuandika Historia leo

Simba Historia Leo Simba SC kuandika Historia leo

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba leo inatarajia kuandika historia wakati jezi mpya za timu hiyo kwa msimu huu zitazinduliwa kileleni mwa Mlima Kilimanjaro zikiwa na majina ya viongozi sita wa serikali ya Tanzania likiwamo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Jezi hizo zinatarajiwa kufikishwa kileleni na kuzinduliwa leo saa 1 usiku tano zikiwana majina ya vigogo hao wa serikalini lakini Jezi ya sita itakayozinduliwa leo itakuwa maalumu kwa Rais wa Heshima ‘Mo’ Dewji, aliyehusika katika usajili wa kishindo wa Mnyama kwa msimu ujao.

Ikumbukwe kuwa hakuna Klabu iliyofanya tukio hili la ufikishaji Jezi katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kama tukio rasmi zaidi ya Simba SC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: