Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens hawana shaka na ubingwa

Simba Er Simba Queens hawana shaka na ubingwa

Tue, 21 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Simba Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), Selemani Makanya, amefunguka kwamba, hawana shaka na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu kwa sababu wamejipanga na wana kikosi imara. Katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), Simba Queens, inashika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 26.

Akizungumza nasi, Makanya alifunguka kwamba: “Hatukuanza vizuri ligi msimu huu kutokana na uchovu wa wachezaji wetu ambao walitoka kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake.

“Lakini baada ya hapo tulirudi kwenye kiwango chetu na pia tulipata fursa ya kuongeza nguvu ya wachezaji wenye uzoefu ndani ya kikosi akiwemo Asha Mwalala pamoja na Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’.

“Tumerudi kwenye nafasi yetu na bila shaka tukiendelea kuweka umakini na kupambana basi hatutotoka kwenye nafasi hiyo na hatimaye tutatwaa ubingwa msimu huu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: