Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Hatuna muda wa kuremba ni kazikazi

Simba SC Squad List Simba: Hatuna muda wa kuremba ni kazikazi

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa sababu kubwa ya benchi la ufundi kutumia mbinu za moja kwa moja kwenye mechi zao za kimataifa ni kutokuwa na muda wa kuremba bali kusaka ushindi.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa: “Katika hatua ya Ligi ya Mabingwa kwenye makundi hakuna muda wa madoido kwa wachezaji kama ambavyo huwa wanafanya akina Clatous Chama, Hennock Inonga kwenye mechi ambazo hazina presha huku ni kazikazi hakuna kuremba.

“Ikiwa wachezaji wataanza kuonyesha madoido watakuwa wanapoteza muda na hayatafanikisha malengo yetu ya kupata pointi tatu. Maamuzi ni kucheza direct football (mpira wa moja kwa moja) anaanza Aishi Manula anampa Shomari Kapombe inapelekwa kwa Chama kisha Saidi Ntibanzokiza.

“Hili la kusema kwamba timu haichezi mpira wa kuvutia hata ikiwa nyumbani hilo halipo kwani timu zote ambazo zinashiriki Ligi ya Mabingwa hizo ni bora na zinacheza vizuri. Mfano mchezo dhidi ya Vipers wachezaji walifanya kazi kubwa lakini hata Vipers nao walikuwa wanakuja kushambulia jambo lililofanya nguvu ya ulinzi iongezeke.

“Horoya wanakuja kwetu na wana tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali hivyo wachezaji wana kazi ya kujitoa kama hakuna mechi nyingine ili washinde na inawezekana mashabiki wajitokeze kwa umakini na muda wa mapumziko upo kwani hakutakuwa na mechi nyingine za kimataifa mpaka Aprili,” alisema Ally.

Ni Machi 18 Simba wanatarajiwa kumenyana na Horoya kwenye mchezo wa kundi C ambpo katika mchezo wao walipokuwa ugenini walitunguliwa bao 1-0.

KUNDI LA SIMBA CAF P W D L GF GA Pts 1.Raja 4 4 0 0 13 1 12 2.Simba 4 2 0 2 2 4 6 3.Horoya 4 1 1 2 2 5 4 4.Vipers 4 0 1 3 0 7 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: