Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba: Asanteni Yanga kwa kutuletea uchochoro

Youssi Uchochoro Winga wa Simba, Pape Ousmane Sakho akifunga bao bora la mwaka mbele ya Yao Attohoula

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga wakilipuka kwa furaha baada ya utambulisho wa Beki wa Kimataifa kutoka ASEC Mimosas ya nchini ni Ivory Coast Yao Attohoula.

Kwa Mashabiki wa Simba wao imekuwa kicheko wakibeza usajili wa Mlinzi huyo wa kulia na kusema mtani (Yanga) amepigwa.

Simba wamekuwa wakitumia picha ya winga wao raia wa Senegal Pape Ousmane Sakho akifunga bao Bora la Afrika mbele ya Beki huyo akiwa na ASEC Mimosas katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Februari 13, 2022.

Sasa Yao Attohoula yupo Jangwani, Je ni kweli uchochoro ama anakwenda kutengeneza ukuta wa zege sambamba na Mwamnyeto, Job, Bacca, Djuma Shaban na Kibwana Shomari.

Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: