Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku ya kumtambulisha namba 6, kuna watu watakata roho - Kamwe

Screenshot 20230707 195121 Opera News Siku ya kumtambulisha namba 6, kuna watu watakata roho - Kamwe

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa siku ambayo watamtambulisha mchezaji wao mpya atakevaa jezi namba 6, kuna watu watafurahi na wengine watapoteza maisha kutokana na mshituko.

Kamwe amesema hayo leo Alhamisi, Julai 13, 2023 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu klabu hiyo.

Mpaka sasa Yanga imetambulisha wachezaji watatu ambao ni Nickson Kibabage (beki na winga kutoka Singida FG), Jonas Mkude (kiungo kutoka Simba Sc) na Gift Fred (beki kutoka SC Villa ya Uganda) huku akitajwa pia winga Maxi Nzengeli kutoka Maniema FC ya Congo DR kuwa huenda akatangazwa leo.

"Wachezaji hawa watatu ambao tumewatambulisha, tayari kuna watu wameanza kukata tamaa, tukimaliza wote, watakata na roho.

"Kama hamjawahi kusikia msiba kwenye soka, mtausikia siku tukitambulisha mchezaji atayevaa jezi namba 6, kutatokea msiba mzito ambapo watu watalia sauti hazitoki machozi yanamiminika.

"Huyu mchezaji atatambulishwa wiki ijayo, saa 6:06 usiku kama ambavyo watu mnakesha kusubiri mwaka mpya, basi siku hiyo mtakesha kusubiri utambulisho wa huyu mwamba.

"Siku hiyo kuna watu wataamka na furaha wakisherehekea ujio wa jezi namba sita lakini wapo ambao watajifungia ndani kwa vilio," amesema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: