Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shikangwa amrithi Opah Clement

Jentrix Shikangwa Jentrix Shikangwa

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa, amemrithi mwenzake aliyekuwa akicheza naye kwenye timu hiyo, Opah Clement kwa kuongoza kwa ufungaji kwenye Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, akifikisha mabao 10 hadi sasa

Opa, ambaye ameuzwa na klabu yake ya Simba Queens hivi karibuni kwenda nchini Uturuki kuichezwa Besikitas alikuwa ndiye kinara wa mabao hadi anaondoka akiwa amecheka na nyvu mara tisa.

Aliyekuwa pacha mwenzake kwenye timu hiyo, Shikangwa raia wa Kenya, amefikisha mabao 10, akiwa amechukua nafasi yake ya ufungaji kwenye kikosi cha Simba Queens na Ligi Kuu pia.

Wakati Shikangwa akiwa na mabao 10, wachezaji watatu akiwamo Opa ambaye pia ni straika wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Twiga Stars, wana mabao tisa kila mmoja.

Wachezaji hao ni Donisia Minja wa JKT Queens na Cynthia Musungu raia wa Kenya ambaye naye ametimkia Uturuki katika timu hiyo ya Opa, akiwa ameacha mabao yake tisa kwenye Ligi Kuu.

Winfrida Charles wa Alliance Girls ana mabao manane, huku wachezaji saba wakiwa na mabao matano kila mmoja.

Wachezaji hao ni Stumai Abdallah, Fatuma Mustapha na Jacline Shija wote wa JKT Queens, Blessing Nkor wa Yanga Princess, Jamila Rajab wa Baobab na Priviledge Mupeti wa Fountain Gate Princess.

Wakati huo huo, timu ya Mbagala Queens imeendelea kufanya kweli kwenye Ligi ya Soka Wanawake Mkoani Dar es Salaam ikifikisha jumla ya pointi 12, ikishinda mechi zote nne ilizocheza.

Msimamo wa ligi hiyo unaonyesha kuwa timu ya Mabibo Queens inashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi tisa, The Eleven Star Queens ya tatu kwa pointi hizo hizo tisa, Sayari Women ikiwa kwenye nafasi ya nne kwa pointi hizo.

Timu hizo tatu zinapishana mabao ya kufunga, huku pia Youngstars Queens ikiwa kwenye nafasi ya tano kwa pointi saba na Evergreen Queens ya sita na pointi saba pia.

Kinondoni Queens inakamata nafasi ya nane ikiwa na pointi nne, Wisdom Queens nafasi ya tisa kwa pointi nne pia, Ubungo Tafseo Queens ya 10 kwa pointi zake tatu.

Tanzanite Princess iko kwenye nafasi ya 11 bila kuwa na pointi, Ukonga Queens ikiburuza mkia nayo ikiwa haina pointi yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: