Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shida ya Yanga itaanzia hapa msimu ujao

Yanga Kombe 2022 23 Wachezaji wa Yanga wakishangili kombe la Ubingwa

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Halina ubishi mastaa wa Yanga walihitaji mapumziko ya muda mrefu, baada ya msimu ulioisha kutumika sana kutokana na ratiba ya kucheza mechi nyingi za michuano mbalimbali waliyokuwa wanashiriki.

Baada ya Ligi Kuu kumalizika (Juni 9) na Yanga kunyakua taji hilo, bado ilikuwa na jukumu lingine la kucheza fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam FC iliyopigwa bao 1-0, ambazo zilichezwa Juni 12, Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.

Wakati Simba ikitolewa robo fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ilifika fainali za Kombe la Shirikisho la Afrika ilicheza dhidi ya USM Alger, jambo lililoongeza uwingi wa mechi walizocheza.

Ratiba nyingine za mechi ni za kawaida kama zilivyokuwa zinashiriki timu nyingine kama Kombe la Mapinduzi na Ngao ya Jamii na Yanga ilifanikiwa kunyakua taji hilo.

MABONANZA

Ni jambo jema na la baraka wachezaji wanapocheza mechi za kuisaidia jamii, ndani ya kikosi cha Yanga ilianzia kwa mabeki Dickson Job na Shomari Kibwana, ambapo walikuwa wanawaalika mastaa mbalimbali ndani ya kikosi chao na nje.

Kikosi cha Kibwana kilikuwa na Metacha Mnata (Yanga), Kibwana (Yanga),Mohamed Hussein 'Tshabalala', (Simba) Bakari Mwamnyeto (Yanga), Lusajo Mwaikenda (Azam FC),Nickson Kibabage alikuwa SBS na sasa Yanga,Mzamiru Yassin (Simba),Simon Msuva (Nje ya nchi),Hassan Dilunga kwa sasa JKT Tanzania na Obrey Chirwa (Ihefu).

Wakati kikosi cha Job ni Beno Kakolanya wakati huo alikuwa Simba na sasa SBS,Israel Mwenda (Simba),Yahya Mbegu anahusishwa na Simba na SBS,Job (Yanga),Hussein Kazi (Geita),Said Ndemla (SBS),Salum Abubakar 'Sure Boy(Yanga),Shiza Kichuya (Namungo), Fiston Mayele (Yanga),Abdul Selemen 'Sopu' (Azam FC) na Danny Lwanga (Geita).

Ukivitazama vikosi vyao kuna mastaa ambao walikwa panga pangua vikosi vya kwanza kama Mayele aliyemaliza na mabao 17 kwenye Ligi Kuu, nahodha Mwamnyeto, Job, Kibwana, Sure Boy,tofauti na kina Zawadi Mauya na Metacha, lakini pia rais wa klabu hiyo, Injinia Said Hersi aliunga mkono juhudi zao kwani alionekana kwenye mechi hizo.

Wachezaji wa Yanga wana mabonanza mbalimbali kama analolifanya Mwamnyeto, Sure Boy alilolifanya Dar es Salaam na Jonas Mkude anahusishwa kutaka kujiunga na timu hiyo.

KWENDA MALAWI

Yanga imealikwa na klabu ya Nyassa Big Bullet ya Malawi kucheza mechi ya kirafiki kwa ajili ya kuadhimisha miaka 59 ya uhuru wa nchini yao, bado hapo kuna safari ndefu nyingine ambayo itawachosha mastaa hao.

KOCHA MPYA

Yanga imeajili kocha mpya, Miguel Angel Gamondi atahitaji wachezaji waingie mapema kambini ambapo inasemekana itakuwa Julai 10, ili aweze kukiona na kuwasoma wachezaji wake, hivyo mastaa hao watakuwa hawajapata mapumziko ya kutosha.

WALICHOSEMA WATALAMU

Staa wa zamani wa timu hiyo, Abeid Mziba anasema kiafya wachezaji wanapaswa kupumzisha miili yao, jambo aliloliona ni kama wanakosa wasimamizi wazuri ambao wangewazuia kuendelea kucheza mabonanza.

"Naomba nieleweke vizuri, mabonanza siyo mabaya, kwani wanafanya upendo dhidi ya jamii inayowazunguka hilo ni jambo jema sana, ila kutokana na muda wao sioni kama wachezaji wa Yanga watapumzika angalau wiki mbili ili kuiipa miili afya.

"Ukiangalia Yanga ina kocha mpya, itategemeana ataanza na mazoezi gani, akianza ya taratibu itakuwa nafuu kwao, ila kama magumu naona kama itawaumiza, siwezi kujua pengine wanafanya hivyo kwa sababu bado umri wao ni mdogo, hivyo wana nguvu ya kutosha, ila nasisitiza kupumzika kwao ilikuwa ni muhimu, kutokana na majukumu mazito waliyokuwa nayo msimu ulioisha."

Mchezaji mwingine wa zamani wa timu hiyo, Bakari Malima anasema wachezaji wanatumia nguvu kubwa, hivyo kuna umuhimu wa kupata muda wa mapumziko ili wanaporejea kwenye majukumu miili yao inakuwa na nguvu mpya.

"Wachezaji wa Yanga walitumika zaidi msimu ulioisha na ndio maana walikuwa na mafanikio makubwa, angalau wangepata muda wa kupumzika ingawa wanachokifanya sio kibaya ni vile ratiba yao inabana."anasema.

Aliyekuwa kocha wa Coastal Union, Joseph Lazaro anasema mapumziko kwa wachezaji ni muhimu kwani wanatumika kwa muda mrefu na kwasababu mechi zinachezwa nyumbani na ugenini safari zinakuwa nyingi.

"Kucheza mabonanza siyo kitu kibaya, ila changamoto inakuja muda walionao kurejea kambini na wanakwenda kwenye mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya ambayo itategemeana na kocha atayaanza ya aina gani."anasema.

Anasema kuna wakati mchezaji anapaswa kwenda mazingira ya mbali na yale anayoyafanyia kazi ili kuipa akili afya ya kuingiza vitu vipya "Kuna wengine wana familia watatakiwa kupata muda wa kukaa nazo, kiukweli mapumziko ni muhimu sana."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: