Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih: Feisal alikosea kuiingizia pesa Yanga

Feisal Salum Fei Toto'' Feisal Salum

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda amesema kuwa alichokifanya mchezaji wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' kuingiza kiasi cha Tsh milioni 112 kwenye akaunti ya klabu yake akidhani kuwa aanavunja mkataba wake kilikuwa ni kinyume na taratibu za FIFA.

Shaffih amesema hayo kufuatia Feisal kugonga mwamba TFF na kuamua kurejea tena kwenye mamlaka hiyo akiomba kuvunja mkataba wake.

"Mimi ni muumini wa taratibu, ninavyofikiri ni kwamba utaratibu unatakiwa kuwa ni Mchezaji na Klabu wakae pamoja na sio lazima mchezaji aende klabuni.

"Zilivyokuwa tetesi za kipindi cha usajili ni kwamba Feisal kusajiliwa na Azam FC na Azam wakathibitisha hilo, Hasheem Ibwe aliongea mahari kwamba yule mchezaji wanaweza wakamchukua.

"Zikaanza taratibu na mchakato ambao ulikuwa unamtoa Feisal Yanga ni kwamba aondoke bure baada ya kutafsiri mkataba wake, ndio maana akaingiza pesa akidhani kwa kufanya vile mkataba wake anakuwa ameununua anaenda kujiunga na timu anayoitaka.

"Baadaye ule mchakato ukashindikana, baada ya kushindikana hakuna sehemu inayooneaha kiliwahi kufanyika kikao cha maridhiano ambacho alikiitisha Feisal na Watu wake kuomba kuondoka zaidi ya barua aliyoiandika ambayo tuliona wote," amesema Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: