Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Yanga ndio Klabu Bora Afrika Mashariki kwa sasa

Shaffih Na Yanga Shaffih Dauda awapa Yanga heshima yao

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba SC ikipenya kwa mbinde na kufika hatua ya Fainali ya Ngao ya Jamii 2023 dhidi ya Singida Big Stars jana Agosti 10 katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Mchambuzi wa Michezo Shaffih Dauda ameongelea baina ya ushindani uliopo kati ya timu hizo nne zinazoshindana katika michuano hiyo huku akiweka wazi kuwa Singida imeimarika na kupuguza wigo wa ubora baina yao na Simba SC ndio maana wameweza kutoa upinzani.

Vilevile Shaffih amewataja Yanga kama Timu bora Tanzania na Afrika Mashariki kwa sasa ndio maana Azam wamekumbana na ugumu kupata matokeo mbele yao;

"Kwangu Mimi timu Bora Tanzania na Afrika mashariki kwa sasa ni Yanga, Kwahiyo Yanga kumfunga Azam kwangu sio story, Kwa mechi ya jana nawaona Singida Fountain Gate wakiwa wamepunguza gape lao na Simba.

"Kingine Jana Singida walikua na Gadiel na Beno ambao hawakuondoka Simba kwasababu hawana kiwango, bali waliondoka kwasababu ya kushindwa kupata nafasi na Gadiel jana alionesha uwezo wake mkubwa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: