Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shaffih Dauda: Mayele ndiye kipimo cha washambuliaji Bongo kwa sasa

Mayele227401 Shaffih Dauda: Mayele ndiye kipimo cha washambuliaji Bongo kwa sasa

Thu, 23 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya michezo nchini ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds Media, Shaffih Dauda amesema kuwa mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo DR, Fiston Kalal Mayele ndiye kioo cha washambuliaji wote nchini kwa sasa.

Dauda amesema hayo kufuatia kazi nzuri anayoifanya Mayele kwenye klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mwili tangu atue Jangwani akiisaidia timu yake kubeba ubingwa msimu uliopita na msimu huu wapo kwenye hatua za mwisho kunyakua tena ubingwa wa Ligi huku wakifanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirkisho Afrika.

Mayele anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara akiwa na mabao 15 wakati kwenye Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na mabao matatu.

"Kwa sasa kipimo cha mshambuliaji kwenye ligi kuu Tanzania bara ni Fiston Mayele, kama ambavyo ilikuwa katika misimu (3) au (4) nyuma kipimo ilikuwa ni Medie Kagere.

"Kwa hiyo Mayele ndio kipimo. Usishangae kuona kila anayefunga anafananishwa nae. Kwa sababu ndio kipimo kilichopo, mfungaji mwingine utamfananisha na nani ili aonekane bora?

"Kwa sababu ili mshambuliaji mwingine aonekane bora lazima umfananishe na Mayele Kwa hiyo Mayele kutumika kama kipimo sio dhambi, kwa sababu tayari ameweka standard.

"Ukitaka kuwa mshambuliaji bora kwenye ligi hii kuwa kama Fiston Mayele," amesema Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: