Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba avaa jezi ya Skudu kwa Mkapa

Skudu Picmm Jezi ya Skudu

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shabiki wa Simba aitwaye Thomas amefichua siri ya yeye kuvaa jezi ya timu hiyo yenye jina la Skudu katika kilele cha tamasha la 'Simba Day' kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza nasi, Thomas amesema Skudu ni mchezaji anayemkubali na haoni shida yoyoye kutumia jina lake licha ya yeye kuishabikia Simba.

"Maendeleo hayana chama, kwangu sio ishu kwa sababu ushabiki wangu Simba haunifanyi kuacha kushabikia mchezaji wenye uwezo mkubwa," amesema.

Aidha aliongeza hadi sasa ameamua kujiita Thomas Skudu na anashukuru mashabiki wenzake wa Simba wamelichukulia jambo la kawaida tu.

"Mwanzoni ilikuwa ngumu kunielewa lakini nashukuru wengi wao wananielewa maana sijaanza kuishabikia Simba leo wala jana."

Skudu Makudubela ni nyota mpya wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambapo usajili wake uliteka hisia kubwa kwa mashabiki kutokana na aina ya utambulisho wake huku akipewa jezi namba sita iliyokuwa inatumiwa na Feisal Salum 'Fei Toto aliyetua Azam.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: