Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senzo aipa siri nzito Yanga kuwamaliza Marumo

Senzo Mbathaaaaaa (600 X 360) Senzo aipa siri nzito Yanga kwa Marumo

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga inashuka Uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa leo kucheza mchezo wake wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini, lakini kuna salamu nzito zimetolewa na bosi wao mmoja wa zamani.

Ujumbe huo umetoka kwa aliyekuwa Afisa Mtendaji wao mkuu, Senzo Mazingisa na ameliambia Mwanaspoti kwa simu kutoka Botswana, anaamini timu yake hiyo ya zamani ina nafasi ya kufika fainali lakini kuna kazi ya kufanya leo.

Senzo ambaye kwa sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu nchini Botswana, alisema Yanga kama wanaishi na ndoto hiyo wanatakiwa kuhakikisha wanashinda vizuri kwenye mchezo wa leo nyumbani ili wamalize kazi.

"Nafuatilia taarifa za Tanzania kaka, unajua hapo nimeishi vizuri na mimi ni Mwananchi kabisa, hii mechi ya kesho (leo) ni muhimu sana kwa Yanga, najua wanacheza na timu ya kwetu Afrika Kusini lakini nafasi yangu nawapa Yanga kushinda," alisema Senzo ambaye aliiachia Yanga mataji matatu msimu uliopita.

"Itakuwa mechi ngumu Marumo sio timu kubwa sana lakini msimu huu wako na matokeo mazuri huku kwenye shirikisho, Yanga kama wanataka kucheza fainali basi washinde hapo nyumbani kwa ushindi mzuri na mkubwa, hapo watakuwa wamewaweza Marumo wasisubiri mechi ya ugenini.

Senzo aliongeza, Marumo sio timu iliyoundwa na wachezaji wakomavu wengi kuizidi Yanga, lakini nidhamu yao ya mchezo ni kubwa huku wakicheza kwa ushirikiano mkubwa uwanjani, ugumu ambao Yanga wanatakiwa kujiandaa kukutana nao.

Alisema kama Yanga itashindwa kushinda nyumbani basi ugenini watakutana na kitu kizito kwa kuwa hesabu za Marumo msimu huu ziko zaidi shirikisho huku pia wakiwa wagumu kufungika nyumbani.

"Nafikiri Yanga wanajua rekodi bora ya Marumo wakiwa nyumbani kama watashindwa kushinda huko Tanzania watakuwa katika wakati mgumu, unajua Marumo haifanyi vizuri nyumbani kwa sasa lakini wamekuwa bora kwenye shirikisho.

"Marumo ni timu inayoundwa na vijana wengi wasio na majina wenye njaa ya mafanikio, utawaona jinsi wanavyocheza kwa nidhamu kubwa kwenye shirikisho nadhani haitakuwa mechi rahisi sana lakini kwangu nawapa nafasi Yanga kushinda kwa kuwa najua kikosi chao na jinsi wanavyocheza nyumbani utaona hata wao pia hawajafungwa nyumbani msimu huu kuanzia ligi ya Tanzania na hata Shirikisho.

"Ningefurahi kuiona Yanga inacheza fainali, unajua nimefanya kazi Yanga ingawa kwetu ni Afrika Kusini na hatua kama hii tuliijenga pamoja ingawa niliondoka njiani, lakini kiwango kikubwa najua ubora na mikakati ya ndani kufika hapa walikofika, nawapongeza viongozi, wachezaji na mashabiki bora wa wananchi wenzangu kwenye hatua kubwa na muhimu kesho."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: