Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sasa ni zamu ya kipa mpya Simba, Ally ajipange

Ally Salim X Lakred Sasa ni zamu ya kipa mpya Simba, Ally ajipange

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Ally Salim, ameanza kupata nafasi ya kuaminika ndani ya kikosi cha Simba, ajiandae kwa ajili ya ushindani kutoka kwa Ayoub Lakrad ambaye ataanza kupata nafasi baada ya kuondoka rasmi kwa Peter Banda.

Ndani ya msimu huu, Salim amedaka mechi nne za mashindano na moja ya kirafiki, hiyo ilitokana na kipa namba moja Aishi Manula kuuguza majeraha kwa muda mrefu.

Mechi tano alizodaka Salim msimu huu ni ya Simba Day dhidi ya Power Dynamos (2-0), mechi za Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate walitoka suluhu ndani ya dakika 90 na kuwatoa kwa mikwaju ya penalti (4-2), dhidi ya Yanga suluhu na kuwatoa kwa mikwaju ya penalti (3-1), mechi za ligi mbili alianza na Mtibwa Sugar (4-2) na ameiongoza Simba dhidi ya Dodoma jiji wakiibuka na ushindi (2-0).

Lakrad ameingia kwenye kikosi cha Simba cha msimu huu baada ya viongozi wa timu hiyo kumalizana na winga Banda aliyepewa mkono wa kwaheri kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya timu hiyo, pia kumpa nafasi Mwarabu huyo.

Banda anaondoka Simba baada ya kuitumikia misimu miwili tangu aingie 2021-23, kitendo kinachompa kipa huyo nafasi kwani idadi ya wageni ilizidi, hivyo rasmi ataanza kucheza.

Simba ina makipa watano, huku namba moja akiwa Aishi Manula anayeuguza majeraha kwa sasa, hivyo Lakrad akionyesha uwezo mambo yanaweza yakabadilika.

Makipa wengine waliopo ni aliyepandishwa kutoka kikosi B, Ahmed Feruz na Hussen Abel aliyesajiliwa kutoka KMC akiwa hajacheza, jambo ambalo wataalamu wa soka wanaona eneo hilo kama litatumika ipasavyo watakuwa na akiba nzuri ya baadaye.

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Yanga, Manyika Peter, alisema Simba kuwepo Abel, Salim na Feruz kunaweza kukawa na manufaa makubwa kwa Taifa kama watawavumilia.

“Kama huyo kipa mgeni ataonyesha ushindani mkubwa, ndiye atakayekuwa anawania namba na Manula akirejea mchezoni, huku waliobakia wakiendelea kuwapa nafasi ya kuwajengea kujiamini zaidi,” alisema.

Hoja yake ilikwenda sambamba na kocha wa makipa wa Mtibwa Sugar, Patrick Mwangata alisema:

”Kwangu bado nampa namba moja Manula ingawa huyo mgeni akianza kucheza ndipo tutakapojua kiwango chake kipoje, ila hao wengine naona wanahitaji muda zaidi kwa timu ya aina ya Simba.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: