Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saleh Jembe: Gamondi tumsubiri Mkwakwani

Gamondi Ms Saleh Jembe: Gamondi tumsubiri Mkwakwani

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' amesema kuwa anamsubiri Kocha wa Yanga, Miguel gamondi kuona mbinu zake katika viwanja vya mikoani.

kauli hiyo ya Jembe imekuja baada ya mchezo wa yanga dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Siku ya Mwananchi huku akianza vizuri kwa ushindi wa bao 1-0.

"Yanga wamenifurahisha kwa sababu ile ilikuwa siku ya burudani, nimeona Gamondi ana vikosi viwili kwa wakati mmoja. Dakika 45 za kwanza ametumia kikosi kimoja na 45 za pili akatumia kikosi kingine, sasa huwezi kuipima timu kwa asilimia 100 kwa dakika 45.

"Lakini nimeona Yanga imecheza vizuri katika ile mechi, kuipima itachezaje kwenye Ligi tusubiri itakapokuja kucheza na timu za Tanzania. Unapocheza na timu ya Afrika Kusini kunakuwa na tofauti kubwa.

"Gamondia atakuwa na mtihani tofauti kwa sababu mechi ya Kaizer ulikuwa Uwanja wa Mkapa ambao ni miongoni mwa viwanja Bora Afrika Mashsariki na Kati, lakini mechi nyingine watacheza Mkwakwani, sasa anatakiwa ajue namna ya kuyakabili matatizo ya Uwanja na kuyafanyia kazi.

"Kingine katika vikosi vyake viwili atatakiwa kuchagua kikosi kimoja, hili ni kutokea kwenye uwanja wake wa mazoezi na mkpizania atakayekutana naye.

"Gamondi kwa mechi hii ametuonyesha yeye ni bora lakini inayofuatia ambayo tutampima vizuri ni pale atakapokutana na timu zetu za Tanzania na mechi za mashindano.

"Yanga wakati wanaanza msimu wa mwaka jana walifungwa na Zanaco ya Zambia, watu wakaanza kusema Yanga hamna kitu lakini waliporudi kwenye ligi wakawa bora mpaka kuchukua ubingwa na kufungwa mechi chache.

"Inawezekana Yanga wametuonyesha soka zuri kwa Kaizer lakini wakashindwa kufanya vizuri kwenye Ligi au wakawa na mwendelezo mzuri, kwa hito tusubiri kuona timu ya gamondi itachezaje.

"Nimemuona Gamondi anapenda soka la kasi na kushambulia ambalo tunatarajia litaleta upinzani mkubwa," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: