Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakho naye aomba kusepa Simba

Sakho Erere.jpeg Sakho naye aomba kusepa Simba

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Mchezaji Pape Ousmane Sakho hawaridhishwi na kukosekana kwa muda wa kucheza kwa Mteja wao ndani ya Simba, wakiamini Msenegal huyo anastahili muda zaidi wa kucheza.

Kutokana na hilo kwa mujibu wa taarifa tulizozipata ni kuwa kuna baadhi ya ofa watazifikisha Msimbazi kumhusu Mteja wao ambazo zitakuwa na maslahi kwa Simba kiuchumi ili Sakho aweze kuondoka kusaka changamoto mpya.

Sakho alisaini kandarasi ya miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, akiwa ametumikia miaka miwili huku kipengele cha mkataba kikimtaka alipe mshahara wa miezi mitatu tu ili avunje mkataba wake, tayari ameshaandika barua.

Wanaamini Kijana anastahili muda wa kucheza zaidi, ijapo mpaka sasa bado hakuna ofa mezani kwa Simba huku zikitarajiwa mwishoni mwa msimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: