Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakho: Simba imenifungulia njia

Pape Sakho TT.jpeg Sakho: Simba imenifungulia njia

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pape Ousmane Sakho ambaye amejiunga na US Quevilly-Rouen ya Ligi Daraja la Kwanza Ufaransa ‘Ligue 2’, ameeleza kuichezea Simba ni kati ya maamuzi bora kufanya katika uchezaji wake wa soka la kulipwa akiwa Afrika.

Winga huyo, alisema kuichezea Simba kumefungulia milango mingi kwake ikiwemo kuwa sehemu ya kikosi cha timu yake ya taifa na kupata shavu la kukipiga Ulaya.

“Nilikuwa na wakati mzuri nikiwa na Simba, nilipata nafasi ya kuonyesha kipaji changu kwenye mashindano ya kimataifa, niliishi vizuri na wachezaji wenzangu ndani na nje ya uwanja kiasi cha kujihisi ni kama nilikuwa nyumbani,” alisema na kuongeza;

“Simba itaendelea kuwa kwenye moyo wangu, ilikuwa ni bahati iliyoje kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa (Senegal), nilikutana na Kaka zangu ambao wanacheza soka Ulaya, kiukweli shauku yangu ilichochea kwa sababu ni ndoto yangu kupiga hatua nashukuru Mungu wakati sahihi umefika.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: