Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sakata la Fei Toto ngoma nzito, Yanga yamuita ofisini

Fatma Karume X Fei Sio Mtumwa Fei Toto

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto' leo Aprili 12 alifika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kujua hatma ya barua yake ya kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.

Fei Toto aliongozana na wakili wake Fatma Karume ambaye baada ya kumaliza kusikilizwa leo amesema kuna vitu vya kisheria vinatakiwa kuwasilishwa Aprili 18 na 25 na Mei 4 ndipo rasmi shauri litasikilizwa tena.

"Tunasubiri Mei 4 tutasikilizwa," amezungumza Karume ambaye aliulizwa kuhusu uelekeo wa sakata hilo na kusema hana chochote cha kuzungumza.

Mkurugenzi wa Sheria Yanga SC, Simon Patrick amesema mpaka sasa bado hawajui muelekeo wa kesi yao na Fei kwa sababu kuna mahitaji ya kisheria ambayo wameombwa kuyawasilisha kwenye Kamati kabla ya kesi kusikilizwa tena.

Aidha, Patrick amesema madai yoyote ambayo Fei anayo hata akitaka kuvunja mkataba, anaweza kufika ofisini kuzungumza.

"Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri," amesema Patrick.

Sehemu ya barua inayotajwa kuandikwa na Feisal Salum kwenda TFF akihitaji kuvunja mkataba na Yanga. Amesema amepitia manyanyaso Jangwani na anaomba akacheze kule anapothaminiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: