Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saido, Mzamiru wamkosha Chama

CHAMA UJUMBE Saido, Mzamiru wamkosha Chama

Sat, 27 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba, Clatous Chama amesema sio jambo kubwa sana kwake kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Chama anasema jambo kubwa kwake ni watu kuona kile anachokifanya kuisaidia timu hiyo na furaha huzidi pale malengo ambayo Simba imejiwekea kwa msimu husika yanapotimia.

Kuhusu suala la Tuzo ya Kiungo Bora msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, anasema amekoshwa na kiwango kilichooneshwa na viungo wenzake wa Simba, Saido Ntibazonkiza na Mzamiru Yassin na kuwatakia kila lenye heri katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo.

"Kwakweli msimu ulikuwa mzuri sana kwetu sisi watatu, kila mmoja amefanya vizuri sana, na amejitahidi kuisadia timu, yeyote atakayeshinda tuzo hii nitakuwa na furaha, " amesema Chama.

Wachezaji wengine wanaowania tuzo hiyo ya kiungo bora ni Bruno Gomes wa Singida Big Stars na Stephan Aziz Ki wa Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: