Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruvu wafunguka kuhusu nyota wao

Valentino Mashaka Kusengama Valentino Mashaka Kusengama

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya taarifa kuenea kuwa klabu kubwa barani Afrika zimeanza kumfuatilia mshambuliaji wa Ruvu Shooting, Valentino Mashaka Kusengama, uongozi wa Ruvu Shooting umeibuka na kusema kuwa endapo klabu hizo zitaridhika nae basi wafuate taratibu husika.

Inasemekana kuwa baadhi ya Klabu zinazomfautilia mchezaji huyo ni pamoja na TP Mazembe, Al Hilal, Al Merreikh na baadhi ya Klabu kutoka nchini Morocco.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alifunguka: “Hizi ni tetesi ambazo nimekua nikiziskia kwa wadau wengi wa soka lakini bado hatujapata mawasiliano kutoka kwa Klabu yoyote kuhusiana na Mashaka.

“Mashaka ni kijana mdogo mwenye ubora mkubwa ambao timu yoyote itatamani kupata huduma yake kwahiyo kama hayo yanayozungumzwa ni kweli basi taratibu zifuatwe na mwisho tutaamua nini cha kufanya.”

Ikumbukwe kuwa Mashaka alijiunga na Ruvu Shooting, Januari mwaka huu katika dirisha dogo la usajili akitokea katika timu ya vijana ya Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: