Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho vs Pluijm, kuna mmoja atanzia mguu wa kushoto

Pluijm X Robertinho Robertinho vs Pluijm, kuna mmoja atanzia mguu wa kushoto

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba ilikuwa na uwezo kabla hata ya usajili kikubwa ni ku-turn up tu kwenye mchezo huu muhimu ambao ndio unaoweza kuwa mwanzo wa kutuonesha kama kweli wamejipanga kurudisha kikamilifu mataji waliyoyapoteza ukiongezea na ubora ulioongezwa.

Singida wameongeza upana kwenye kikosi chao na ndipo ubora wao ulipo. Inawezekana wakaongezea nguvu pale walipokwama kidogo msimu uliopita. Ubora wenye muendelezo ulikuwa haba kwenye kikosi chao msimu uliopita.

Mwalimu Robertinho anaanza kuhesabiwa sasa, Jumapili ilikuwa ni michezo na furaha, presha iliopo kwake ni kubwa hasa kutokana na namna ambayo anaonesha kumudu ukubwa wa kikosi chake na wachezaji anaochagua kuwatumia.

Hans Van Der Pluijm hapewi nafasi lakini haina maana kuwa hana presha, Singida wamewekeza sana na anaweza asipigiwe kelele nje na mashabiki lakini ndani watu wanaunguza mifuko wakiwa wanaamini yeye ni mtu sahihi.

Hii ni do or die, Robertinho anaweza kuanza kuponzwa hapa na Hans anajua hili ni kombe ambalo kiuhalisia wanaweza kuwa na nafasi ya kulipambania kama kweli wanataka kuwa wakubwa kama biashara walioifanya inavyotuonesha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: