Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho awabadilisha mbinu Wazambia

Robertinho Sersss Robertinho awabadilisha mbinu Wazambia

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema kuwa ataingia na mbinu tofauti watakapovaana dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia.   Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.   Timu hizo hivi karibuni zilicheza mchezo wa kirafiki katika Tamasha la Simba Day lililofanyika kwnye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0.   Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia, mabao ya Simba yalifungwa na viungo wapya Willy Onana na Fabrice Ngoma.   Akizungumza kuelekea mchezo huo Robertinho alisema kuwa ametumia muda mwingi kuwasoma wapinzani wao Power Dynamos, hivyo hana hofu kuelekea mchezo huo.   Robertinho alisema kuwa ataingia kitofauti kuelekea mchezo huo kwa kubadili mbinu, mfumo na wachezaji atakaowatumia katika mchezo hao kwa lengo la kuwavuruga wapinzani wao.   Aliongeza kuwa anaamini Benchi la Ufundi la Power Dynamos, wataingia kwa staili waliyoitumia katika mchezo huo wa kirafiki waliocheza, kwa kuzuia viungo watawale eneo la kiungo ambapo ameliona hilo na amepanga kulifanyia maboresho kuelekea mchezo huo.   “Mchezo tuliokutana nao katika Tamasha la Simba Day ulikuwa na makusudi tofauti, huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika nao ni tofauti, huu ni mchezo wa maamuzi.   "Nimetumia muda kuwasoma wapinzani wetu na tayari mikakati imekaa sawa tunasubiri siku ya mchezo, kikosi changu kipo fiti na tayari kupambana kupata matokeo mazuri katika mchezo huo wa ugenini,” alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: