Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho atuliza presha Simba SC

Robertinho Vipers Simba Robertinho atuliza presha Simba SC

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amekiri kuwa kikosi chake hakikuwa na wakati mzuri kwenye mchezo huo na kutamba watabadilika na kuonesha soka safi dhidi ya Horoya AC.

Simba Jumanne iliyopita walikuwa wenyeji wa Vipers katika mchezo wa Kundi C wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, ambapo Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi sita na kupanda mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi C, kama watafanikiwa kuifunga Horoya AC, watakuwa wamekata tiketi ya kutinga robo fainali ya mashindano hayo.

Akizungumza nsi, Robertinho alisema: “Ulikuwa mchezo mgumu kwa kuwa wapinzani wetu walikuja na lengo moja tu, la kuzuia na kucheza kwa namba kubwa nyuma ya mpira.

“Hii ilitupa wakati mgumu kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini nashukuru kwa kuwa tumefanikiwa kushinda na kupata pointi tatu muhimu ambazo zimetusogeza hatua moja kutimiza malengo yetu ya kucheza angalau nusu fainali.

“Najua hatukucheza vizuri kama ambavyo mashabiki wetu walitarajia, lakini tunawaomba watulie kuna vitu tutarekebisha kuelekea mchezo dhidi ya Horoya.”

Mechi ijayo Simba atacheza na Horoya ya Guinea katika raundi ya tano ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika kwenye Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: