Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho ashusha presha Simba

Robertinho  Instagram Robertinho ashusha presha Simba

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira amefichua mpaka sasa hana presha yoyote juu ya safu yake ya kiungo kutokana na ubora mkubwa unaonyeshwa na viungo wake wa kati, Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma hali inayopelekea kupata ugumu wa chaguo la kwanza.

Ikumbukwe kwamba Simba ilipishana na taji la ligi msimu wa 2022/23 liliobukia Jangwani pamoja na Ngao ya Jamii pia ilikwenda Yanga.

Msimu wa 2023/24 ni Yanga wamekuwa mashuhuda wa Simba wakitwaa Ngao ya Jamii kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Robertinho ametoa kauli hiyo kutokana na ubora wa viungo hao katika eneo la kati kwa kuweza kuituliza timu na kuweza kutengeneza mashambulizi ambapo mpaka sasa Simba imefanikiwa kushinda mechi nne za mashindano zikiwemo mbili za Ligi Kuu Bara.

Robertinho amesema kuwa ubora mkubwa unaonyeshwa na safu yake ya kiungo cha kati kinapelekea kutokuwa na mchezaji mwenye nafasi ya uhakika kutokana na wote kuwa kwenye ubora unaofanana katika kutekeleza majukumu ya timu ndani ya uwanja.

“Timu ipo kwenye wakati mzuri kwa ajili ya mashindano ambayo yapo mbele yetu kutokana ukubwa wake, ukiangalia tuna Ligi ya Mabingwa Afrika, Super League, Kombe la FA pamoja na michuano ya Mapinduzi.

“Lakini napata furaha zaidi kwa sababu karibu kila idara wachezaji wamekuwa wakionyesha ubora wa kiwango kikubwa ambacho kinachangia kupata matokeo mazuri.

“Hakuna ambaye anaweza kusema anaweza kuwa na nafasi ya kudumu ndani ya timu yangu kwa sababu wote wamekuwa katika ubora mkubwa, angalia eneo la kati kuna Mzamiru, Ngoma pamoja na Sadio Kanoute, ambao wote wanaisadia timu kwa kutimiza majukumu yao kwa kila ambaye anayepata nafasi ya kucheza,” amesema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: