Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho aifungia kazi Wydad

Robertinho Hgs.jpeg Robertinho

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema kwa sasa wameshasahau mechi ya Yanga na wanajiandaa kuwamaliza Wydad Casablanca kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar, mchezo utakaoshuhudia matumizi ya VAR, teknolojia ya video itakayomsaidia refa iliyoletwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Simba itavaana na Wydad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika, hatua ya robo fainali Jumamosi ijayo ikiwa ni wiki moja tangu walipowachapa watani wao wa jadi Yanga mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu Bara.

Simba inakutana na Wydad Jumamosi hii na kocha Robertinho amesema ushindi tu ndiyo tageti yao.

"Kila mmoja wetu anatambua tuna mechi ngumu zinazokuja mbele yetu, hivyo tunahitaji kuhakikisha tunacheza kwa kasi ile ile kwenye kila mchezo, sasa ili kufanikisha hilo ni lazima tujiandae vizuri kimwili na kiakili, akili yetu inafahamu tunatakiwa kuumaliza mchezo hapa Dar na kwenda ugenini tukiwa na kitu mkononi."

Aidha Robertinho aliongeza ipo programu maalumu aliyoiandaa kwa mastaa ambao hawakubahatika kucheza mchezo wa 'Derby' ili kutengeneza fitinesi nzuri na bora itayowaweka katika hali nzuri ya kiushindani na wengine.

"Tunatambua malengo yetu kama klabu na sisi kama benchi la ufundi tunaandaa vizuri timu kwa ajili ya michezo ijayo, hatuna kisingizio kwa sababu huu ni wakati wa kuonyesha uwezo wetu kwa wapinzani waliokuwa mbeleni ambao tunafahamu ubora wao."

Robertinho aliongeza kucheza na timu mbalimbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hadi sasa kumeongeza kitu kikubwa kwa wachezaji wa kikosi hicho hasa jinsi ya kujiandaa kupambana na mastaa ambao wana majina makubwa.

"Kucheza na Raja Casablanca, Horoya, Vipers ni dhahiri kuna kitu kikubwa wachezaji wanapata lakini hata sisi benchi la ufundi kwa maana ya kukutana na mbinu tofauti ambazo zinatuongezea ufanisi kwenye kazi," alisema.

Wydad ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii wamechukua taji la CAF mara tatu kuanzia mwaka 1992, 1975 na 2022 na ilimaliza ya pili katika miaka ya 2011 na 2019 huku mara ya kwanza kukutana na Simba ilishinda 3-0 mwaka 2011.

Katika kundi A, Wydad ilimaliza kinara na pointi 13 ikipoteza mechi moja tu ikicheza ugenini dhidi ya JS Kabylie ya Algeria, ikishinda nne na kutoka sare moja huku kwa upande wa Simba ikimaliza ya pili kundi C na pointi tisa.

Kinara wa mabao Simba ni Clatous Chama mwenye manne wakati kwa Wydad ni mshambuliaji raia wa Senegal, Bouly Sambou mwenye matatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: