Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho aenda na Chama, Saido msimu huu

Chama Saido Mlk Chama na Saido

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amesema kikosi chake kina makundi mawili, moja kati yao lipo tayari kwa ajili ya ushindani huku akisisitiza Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza watacheza sana msimu huu.

Robertinho alifunguka hayo siku moja baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Power Dynamos kwenye mchezo wa kirafiki wa kutambulisha kikosi cha msimu mpya, uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye Tamasha la Simba Day.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, alisema wachezaji wake kwa asilimia kubwa wamefanya kile alichokuwa anakitarajia huku akikiri amefanikiwa kuunda makundi mawili kutokana na uwezo wa wachezaji wake na sasa anaamini mashabiki wataielewa timu yao.

“Tulikuwa na wiki tatu nzuri Uturuki, siku saba za kwanza zilikuwa ni mazoezi ya viungo na nguvu, za pili ni mazoezi ya kuchezea mpira na wiki ya tatu tulicheza mechi za kirafiki zilizonipa mwanga wa kutambua wachezaji walio fiti tayari kwa mchezo, nafikiri kila mmoja sasa atakubali tuna kikosi kizuri na kipana;

“Simba ina kikosi kizuri, wachezaji wamecheza vizuri lakini napenda kuweka wazi nimegawa wachezaji katika makundi mawili, tayari nina kikosi kilicho tayari na kingine kinahitaji muda zaidi ili kiweze kuendana na kasi ninayo ihitaji.”

Alisema wachezaji wote wamecheza vizuri isipokuwa kuna waliofanya mambo makubwa ambayo hakutarajia akimtaja kiungo mkabaji Fabrice Ngoma na mshambuliaji Willy Onana ambao alisema bado wanahitaji muda zaidi ili kuonyesha uwezo mkubwa zaidi walionao.

“Onana kapata dakika chache na kaonyesha kitu kizuri kwa kufunga bao lililowarudisha mchezoni, Ngoma alipoingia akitokea benchi pia alionyesha mchezo mzuri na kufanikiwa kufunga, hao bado pia wanahitaji muda kuwa fiti zaidi ili kuonyesha mambo makubwa,” alisema.

Akimzungumzia Chama na Saido alisema mastaa hao ndio mhimili wake wa timu hivyo wataendelea kuonekana sana kwenye kikosi chake japo anaendelea kuwaweka fiti mastaa wapya ili wasaidiane.

“Tayari nina muhimili wangu wa timu hivyo wadau wa soka wasitarajie mabadiliko katika hilo kwa sababu Chama, Saido, Henock Inonga, Mzamiru Yassini ni wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wamekuwa na mchango kwenye timu na nataka kuwahakikishia watacheza sana msimu huu pamoja na kuwa tumesajili wengine.”

Hawa wana uzoefu kwenye timu na wanafahamu ni kitu gani tunakihitaji, wameshafanya vizuri mazoezini na naamini kwenye michezo ijayo bado watafanya mambo makubwa,” alisema kocha huyo raia wa Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: