Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho achimba mkwara Yanga: Napenda sana Dabi

Robertinho Kuelekea Robo Robertinho atupa dongo zito Yanga

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa imebaki takribani wiki moja kabla ya Simba na Yanga kucheza mechi yao ya pili ya dabi msimu huu, Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robetinho’ ametoa kauli nzito kuhusu mechi hiyo.

Robetinho amesema Aprili 16 kwenye Uwanja wa Mkapa, wanakwenda kucheza na Yanga, ila yeye kwake anaona ni jambo la kawaida kwani mechi za dabi anazipenda na uzuri Yanga anawajua na ameshawahi kuwafunga.

Akizungumzia mchezo huo, Robertinho alisema; “Napenda sana dabi, hizi ni mechi nzuri sana kwangu, kwa bahati nzuri nimewahi kuwafunga Yanga kwa hiyo hawanisumbui, sina wasiwasi nao kabisa. Tunakwenda Mbeya kwanza.

“Tukirudi huko, tutaanza maandalizi ya kucheza na Yanga kisha tutaanza kujipanga kucheza na Wydad. Mechi zote hizi ngumu na muhimu kwetu kushinda,” alisema.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Robertinho kwenye dabi ya Simba na Yanga, huku akiwa na rekodi ya kuwafunga Yanga wakati akiwa anaisimamia Vipers ya Uganda kwenye mechi ya kirafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: