Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Sasa mleteni yeyote, kosi lipo tayari!

Robertinho Sersa Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amesema kikosi chake amekiandaa vizuri na kipo tayari hivi sasa kucheza na timu yoyote.

Kauli hiyo ameitoa juzi mara baada ya kuripoti katika kambi ya timu hiyo iliyopo katika Mji wa Ankara, Uturuki, wakijiandaa na msimu ujao a 2023/24. Kocha huyo aliondoka kwa takribani wiki moja kwenda kwoa Brazil, kabla ya kurudi hivi karibuni.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema yupo tayari kupambana na timu yoyote kwa sasa kutokana na usajili ambao wameufanya vongozi kupitia ripoti yake.

Robertinho alisema kingine amefurahia ubora na kiwango cha kila mmoja ambacho amekionesha mazoezini na katika mchezo wa kirafiki waliocheza juzi dhidi ya Zira FC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Aliongeza kuwa, alichobakisha hivi sasa ni kuwaongezea vitu vichache vya kimbinu wachezaji wake ikiwemo safu ya ushambuliaji ambayo nusu ya wachezaji wamesajiliwa hivi karibuni.

“Nimekaa siku chache na timu hapa kambini Uturuki, nichukue nafasi hii kuwapongeza viongozi wangu kwa kuniletea wale wachezaji waliokuwepo katika mipango yangu ya msimu ujao.

“Usajili huu unanifanya nitambe kuwa tupo tayari kucheza na timu yoyote tutakayokutana nayo katika mashindano yatakayokuwepo mbele yetu wakati tukijiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimefurahi kuona uwezo wa kila mchezaji katika mchezo uliopita wa kirafiki ambao tumecheza dhidi ya Zila FC, kila mmoja alionesha kiwango bora hali itakayonipa ugumu wa kupanga kikosi kutokana na ubora wa wachezaji wapya waliosajiliwa,” alisema Robertinho.

Kikosi cha Simba Agosti 2, mwaka huu, kinatarajiwa kurudi Dar kutoka Uturuki, tayari kwa ajili ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 6, 2023, huku ikianza msimu wa 2023/24 kwa kucheza nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate, Agosti 10, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: