Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Nakuja na mifumo mitatu, hakuna atakaepona

Robertinho Simba G Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Robertinho amefunguka kuwa kambi yao ya Uturuki imekuwa na manufaa makubwa kwani sasa amepata mifumo Mitatu hatari ambayo Simba inaweza kutumia katika michuano yote kwa msimu unaoanza mwezi ujao.

Robertinho alisema mifumo hiyo imetokana na upana wa kikosi chake kufuatia ujio wa mastaa bora ambao wamekuja na nguvu kubwa kuunganisha na wale ambao wamewakuta.

Hata hivyo Kocha huyo alikataa kuanika mifumo hiyo kwa kusema ni sawa na kuuza siri za kambi ya vita, lakini akasema ataitesti kwenye mechi ya Tamasha la Simba Day dhidi ya Power Dynamos kabla ya kuhamishia kwenye Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: