Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Robertinho: Huyu Luis Miquissone! bado kidogo

Robertinho X Jose Luis Miquissone Robertinho: Huyu Luis Miquissone! bado kidogo

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Kocha wa Simba Roberto Oliviera "Robertinho" amesema hana wasiwasi na winga Luis Miquissone na tayari wameshamuandalia winga huyo programu maalumu itakayorudisha kiwango chake na kasi yake ambayo ataitekeleza sambamba na wachezaji wenzake ambao walichelewa mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya kule Uturuki.

“Luis ni mchezaji mzuri nampenda anajituma sana unajua hii ni mechi ya kwanza na kuna mambo ambayo nilizungumza naye atahitaji muda kidogo kujirudisha kwenye ubora wake. Kitu bora ambacho watu wanatakiwa wafahamu huyu n mchezaji ambaye amerudi kuwatumikia Wanasimba anajituma sana ni mpambanaji na mshindani nidhamu hii itamrudisha haraka kwenye kiwango chake.

“Kuna programu tumeitengeneza ambayo atafanya yeye na wenzake wote waliochelewa kambi ya Uturuki baada ya muda atakuwa sawasawa kucheza vizuri zaidi.

Chanzo: Dar24
Related Articles: