Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rivers United: Tumefurahi kupangwa na Yanga

Sdf 076681 Rivers United: Tumefurahi kupangwa na Yanga

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa kikosi cha Mabingwa wa Soka nchini Nigeria Rivers United, Morice Chukwu ameitahadharisha Young Africans kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Rivers itaialika Young Africans nchini Nigeria Aprili 23, katika Uwanja wa Yakubu Gowon kabla ya mchezop wa Mkondo wa pili ambao utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam April 30.

Chukwu amesema hawaogopi kukutana na timu yoyote kwani wamejiandaa vya kutosha na lengo lao ni kuhakikisha wanafika Fainali katika Michuano ya Kombe la Shirikisho na kutawazwa kuwa Mabingwa msimu huu 2022/23.

Rivers imefanikiwa kuonyesha kiwango cha juu kwenye michezo ya hatua ya Makundi ikiwa na mastaa wapya kama mabeki Ngwen Ndasi, Lawrence Edward, viungo wa kati Joseph Onoja, Ukeme Williams na mshambuliaji Nyima Nwagua.

Kiungo huyo mshambuliaji amesema wanaiheshimu Young Africans na wanafahamu mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa upande wao kutokana na wapinzani wao kuwa na kikosi kizuri na kocha wao anawasisitiza na kuwajenga kuwa imara kutokana na ukubwa wa mchezo huo.

Kiungo huyo amesema wamejipanga kushinda na wanaendelea kufanya mazoezi ya nguvu ili kuhakikisha wanakuwa vizuri kila idara maana lengo lao ili litimic lazima wawe na maandalizi ya kutosha.

“Binafsi naombea nisipate majeraha ili niweze kucheza mechi zote mbili ili niwe mmoja wapo wa watakaoweka historia ya kuifunga timu bora kama Young Africans,”

“Nilifurahi sana niliposikia tunakwenda kukutana na Young Africans kwa sababu tulishawahi kucheza nao hivyo ninajua kiwango chao,” amesema Chukwu

Wapinzani hao walishawahi kukutana mwaka 2021 katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Afrika, Rivers walitembeza kichapo cha nje na ndani kwa kuwapiga jumla ya mabao 2-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: