Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ratiba kamili ya Yanga Nigeria iko hivi

Yanga Hgs.jpeg Ratiba kamili ya Yanga Nigeria iko hivi

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimeanza safari leo Alhamisi, Aprili 20, 2023 kuelekea Nigeria kuwafuata Rivers United kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wamepitia Addis Ababa, Ethiopia kabla ya kutua kwenye Uwanja wa Murtala Muhammed International Airport jijini Lagos majira ya saa 6:30 mchana.

Watapumzika jijini hapo na kisha kufanya mazoezi mepesi jioni ya leo.

Safari ya saa 1 na dakika 30 kuelekea Uyo, kwenye Jimbo la Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria ambapo ndio mechi inachezwa itaanza kesho Ijumaa saa 3 asubuhi, kwa usafiri wa ndege za ndani ya Nigeria.

Baada ya kuwasili Uyo, kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi ili kujiandaa na mchezo utakaopigwa Jumapili tarehe 23, kwenye dimba la Godswill Akpabio majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: