Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais awatoa hofu Mashabiki Yanga "Haondoki mtu"

Nabi Na Rais Hersi Said Rais wa Yanga, Injinia Hersi sambamba na Kocha Nasreddine Nabi

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga,Eng Hersi Said amewatoa hofu mashabiki wote wa Yanga wanaotetemeshwa na taarifa za kutimka kwa Kocha kuwa wanatambua kazi nzuri ambayo inafanywa na benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha mkuu Nabi.

Hivyo sisi kama Viongozi hatupo tayari kuona kocha yoyote ambaye yupo Kwenye benchi letu la ufundi anaondoka kwa sasa,Tunaendelea kuijenga Yanga imara kwa sasa.

Bado tuna malengo, mipango endelevu na Kocha Nabi hivyo hatoweza kuondoka kwa gharama yoyote licha ya ofa nyingi zipo mezani kwetu kumuhitaji kocha wetu Nabi.

Wananchi hawapaswi kuwa na woga wowote Nabi ataendelea kuwepo Yanga.Tupo ukiongoni kumaliza Mashindano ya ndani Kama Ligi kuu NBC na kombe la FA na Kimataifa tupo hatua nzuri kwenda fainali.

Kila siku sisi Kama Viongozi tunakumbushana majukumu yetu pamoja na wachezaji wetu wote ambao tupo nao kambini Zawadi kubwa pekee kwa mashabiki wetu ni kuwapa Zawadi ya ubingwa tu hakuna kingine.

Kuhusu Usajili

Bado ni mapema kuzungumzia usajili kuelekea msimu ujao ila kwa sasa tunamalizana kwanza na wachezaji wetu wote ambao kocha anataka kuendelea nao.Ila msimu ujao hatutafanya usajili mkubwa sana ila wachezaji ambao watakuja watakuwa wazuri kuja kuisaidia Yanga.

Kuhusu Uwanja

Hili naomba wanayanga wote wajue ni deni kwangu Kama ahadi yangu kwao,nitakuwa sina cha kujibu mbele za Mungu Kama nitashindwa kutimiza ahadi hii.

Malengo yetu ya uwanja yapo palepale na ndani ya mwaka huu nyie wenyewe mtaanza kuona siwezi kuwambia ni lini ila ndani ya mwaka huu tutaanza utekelezaji huu wa uwanja wetu pale jangwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: