Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yanga akosa usingizi saini ya Makabi Lilepo

Makabi Lilepo Ms Makabi Lilepo

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imeshtua kwa kumpiga chini winga, Bernard Morrison ambaye mwishoni mwa msimu huu alianza kuwaka, lakini hawakujali hilo na wakampa 'thank you' ili akasake klabu nyingine, wakati Mghana huyo anatoka kuna vuma viwili wataingia fasta.

Hesabu kali za Yanga baada ya kumpiga chini Morrison bosi wao mkubwa wa klabu, Injinia Hersi Said ambaye ndiye stelingi wa vita ya usajili kuna hesabu kubwa anaweza kuzipiga kufuatia kupatikana nafasi ya Morrison.

Morrison akiwa Yanga ndiye aliyekuwa analipwa fedha ndefu akichukua Dola 10,000 (Sh 23 milioni) kwa mwezi hatua ambayo mabosi wa Yanga wanaona kazi aliyoifanya kwa msimu uliopita haiendani na kiasi alichokuwa anachukua.

Yanga sasa wanataka kutumia mshahara huo wa Morrison kuipigania saini ya winga Makabi Lilepo wa Al Hilal ya Sudan ambaye walikuwa wakishindana naye mshahara.

Endapo Yanga watafanikiwa kumnasa Lilepo watakuwa wameziba nafsi ya Morrison kwa mtu wa maana ambaye atawaongezea ubora mkubwa kwenye safu yao ya ushambuliaji kwa msimu ujao. Mwanaspoti linafahamu kwamba Hersi yuko kwenye mawasiliano mazuri na Lilepo sio kwasasa pekee hata kabla ya kutua Sudan aliwahi kuhitaji huduma yake akiwa klabu yake ya zamani ya AS Vita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: