Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia amaliza utata Simba kucheza Fainali CAF 1993

Rai Samia Ndege Rais Samia Suluhu Hassan

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 05,2023 ameshiriki chakula cha usiku Ikulu Dar es salaam na Timu ya Yanga kwa ajili ya kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) ambapo kwenye salamu zake za pongezi amesema historia inaonesha Timu za Tanzania zinafanya vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa na kwamba mwaka 1993 Timu ya Simba nayo ilifika katika hatua ya Fainali ya Kombe la CAF.

“Yanga kufika Fainali za mashindano haya kumeiletea Tanzania heshima na kuturejesha kwenye ramani ya kisoka, mara kadhaa nilikuwa nasema nataka kuirudishia Tanzania heshima yake ikae pale inapotakiwa kukaa, sasa upande wa michezo Tanzania imerudi kwenye ramani yake”

“Kufika hapo haikuwa kazi rahisi Nchi nyingi zilishikiri hata sisi tuliingia moja ikatoka nyingine ikaendelea, niwaombe sasa Viongozi muendelee kuwapa ari, hamasa na motisha Vijana wetu hata kwa kuangalia maslahi yao, wanasema chanda chema huvishwa pete kawavisheni pete Vijana”

“Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuongeza juhudi za kuendelea kujitayarisha kwa michuano yote ya Kimataifa inayokuja ili tufanye vizuri, historia inaonesha Timu zetu hizi zinakwenda na zinafanya vizuri, mwaka 1993 Timu ya Simba nayo ilifika katika kiwango hicho”

“Sasa nimewajua Simba akina nani?, nilikuwa namuuliza Naibu Waziri Khamis Mwinjuma (Mh. FA) kwamba Karia ni Timu gani akajibu Coastal nikamwambia hapana Karia ni Simba lakini na yeye mwenyewe Naibu Waziri (FA) ni Simba, Nchi yetu inaweza kufanya vizuri kinachotakiwa ni matayarisho na hamasa tujipange tukafanye vizuri”

View this post on Instagram

A post shared by Dozen’s Selection (@dozenselection)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: